Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:17

Mahakama kuu Marekani yakataa rufaa ya Ali Samantar wa Somalia


Mahakama Kuu ya Marekani
Mahakama Kuu ya Marekani

Mahakama kuu ya Marekani, imekataa rufaa ya waziri mkuu wa zamani wa Somalia, ambaye alitakiwa kulipa dola milioni 21 kwa waathirika wa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini mwake.

Mahakama hiyo imekataa kupitia maamuzi ya mahakama ndogo ambayo inakubali kuendelea kwa mashtaka dhidi ya Mohamed Ali Samantar.

Alihudumia kama waziri mkuu na waziri wa ulinzi katika uongozi wa dikteta wa Somalia, Mohamed Siad Barre, katika miaka ya 1980 na mwanzoni mwa 1990.

Mahakama ya serikali kuu ya Marekani inamuona Samantar, ambaye anaishi katika jimbo la Virginia, hawezi kuwa na kinga kwa kuwa alikuwa kiongozi katika nchi ya kigeni.

Naye mwanasheria wake ameiomba mahakamakuu kufikiria maamuzi ya mashtaka ya Samantar.

Mwaka 2012 mahakama ya wilaya ilimuamuru Samantar, kulipa dola milioni 21 kwa wale walionyanyaswa na maafisa chini ya utawala wake.

XS
SM
MD
LG