Wakulima kutoka county ya Nakuru, walifunga njia kuu kati ya Nairobi na Naivasha kwa muda mrefu siku ya jumatatu kupinga mradi wa kujenga mitanbo ya kuazalisha umeme kwa kutumia upepo.
Wakulima kutoka shamba la Kinangop Wind Park walifunga njia kuu wakiitaka serikali kuzuia mpango wa kujenga minara mirefu yenye feni kubwa ambazo zikisukumwa na upepo zinasukuma mitambo inayozalisha umeme.
Waziri wa nishati, mali asili na maji wa County ya Nakuru Richard Rip alipatikana katika msongamano wa magari ulokuwa na urefu wa karibu kilomita 10, ameiambia sauti ya amerika kwamba tatizo linatokana na watu wanaowapotoshwa wakulima kwamba mitambo hiyo itakuwa na madhara kwa mashamba yao, mifugo na hata afya yao.
Bw. Rip anasema madai hayo hayana msingi na kwamba wamekubaliana na wakulima, wakuu wa serikali na wawekezaji wa binafsi wa mpango huo kwamba mradi huo utakuwa na faida kwa wakazi wa eneo zima kwani utazalisha megawati 60 za umeme ukimalizika.