Ndovu wa Ivory Coast wanyakua Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya mikwaju 11 ya penalty na kuishinda Ghana ambayo ilikua inaongoza katika mikwaju hiyo, mjini Bata, Equatorial Guinea.
Baada ya dakika 120, si wachezaji Ghana wala wale wa Ivory Coast waloweza kuliona lango ingawa kila upande ulikosa mabao mazuri katika wakati wa muda huo wote.
Hatimae ilikuwa ni mikwaju ya penalti ndiyo iliamua mshindi pale Ivory Coast iloiweza kuilaza Ghana mabao 9 kwa 8. Na hapa historia kujirudia tena, kwani miaka 23 iliyopiota timu hizi zilikutana katika finali ya Kombe la Afrtika na ni mikwaju ya penalti ndio iliamua mshindi ambapo vijana wa Ndovu walinyakuwa kombe.
Nyota wa mchezo ni kipa wa Ivory Coast, Copa Barry, kwani mikwaju ya penalti ilibidi hadi makipa kupiga na Copa alizuia mkwaju wa mwenzake wa Black Star Braimah Kamoko, na kutumbukiza wavuni bao lake la ushindi.