Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:17

DRC yachukua ushindi wa nafasi ya tatu ya AFCON 2015


CAN Mashabiki wa DRC wakiangalia ikiwa timu yao itailaza Congo walipokua sare 2-2
CAN Mashabiki wa DRC wakiangalia ikiwa timu yao itailaza Congo walipokua sare 2-2

Vijana wa Leopard wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wamefanikiwa kuwalaza wenyeji Nzalanga wa Equatoria Guinea, katika mchuano ambao wachezaji wa pande zote mbili walionekana wamechoka.

Mchuano huo ulofanyika mjini Malabo, mji mkuu wa Equatorial Guinea haukuwa wa kusisimua kwani ilionekana wachezaji wamechoka na hasa uwanja ulikuwa mtupu, mashabiki hawakuvutiwa sana na hasa kufautia ghasia zilizotokea katika nusu finali.

Ilihitaji mikwaju ya penalty kwa DRC kupata ushindi wa mabao manne kwa mawili na kuweza kurudi nyumbani wakiwa na medali ya tatu ya Kombe la mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu 1998.

Wenyerji Equatorial Guinea wameridhika na matokeo hayo kwani ni mara ya kwanza katika historia ya nchi yao kuweza kuwasili katika daraja hiyo, na kuonekana kuwa na matumaini ya kuwa timu itakayoheshimiwa katika kandanda barani Afrika.

XS
SM
MD
LG