Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inakuwa timu ya kwanza kuingia katika nusu finali ya kombe la Mataifa ya Africa, nchini Equatorial Guinea baada ya kuwalaza ndugu zao wa Congo mabao manne kwa mawili siku ya Jumamosi.
Congo iliweza kutia mabao mawili katika muda wa dakika sita katika kipindi cha pili lakini vijana wa DRC waloamua kutoshindwa walirudisha mabao mawili na kuchukua ushindi katika dakika za majeruhi.
KOcha Jean Florent Ibenge anasema alikuwa na imani na vijana wake na alifahamu jinsi Wacongo walivyokuwa na furaha na kujisahau walipokuwa wanaongoza mawili kwa bila.