Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 18:48

CAF: Bahati nasibu kuamua mshindi wa kundi D


Michel Dussuyer, kocha wa Guinea akizungumza na wandishi habari baada ya mchuano na Mali
Michel Dussuyer, kocha wa Guinea akizungumza na wandishi habari baada ya mchuano na Mali

Kwa mara ya kwanza tangu 1988, uwamuzi wa timu kusonga mbele kuingia katika robo finali ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON utachukuliwa kwa bahati nasibu.

Shirikisho la Kandana Africa CAF limetangaza Jumatano usiku kwamba zowezi litafanyika chini ya kifungu cha 74 cha katiba ya CAF na kufanyika Alhamisi saa kumi jioni mjini Malabo, baada ya Mali kwenda sare 1 kwa 1 na guinea.

Makocha wa timu zote mbili Michel Dussuyer wa Guinea na Henri Wajelech Kasperczak, wanakubali kwamba mchuano wao haukufikia kiwango cha uwezo wa timu hizo mbili, hasa upande wa Mali baada ya kapteni Syedu Keita kukosa mkwaju wa penalty katika nusu ya kwanza.

“Hatuna budi, hiyo ndio sharia inabidi kuheshimu. Lakini nina amini kunahitaji mabadiliko katika sharia hiyo maana si dhani ni uzuri au haki kuamua matokeo ya kandanda kwa kupiga kura au watu kukaa mezani kuamua, sharia inabidi kubadilishwa,” amesema Bw Kasperczak

Katika mchuano wa pili wa Jumatano, Kundi hili la D Ivory Coast ilifanikiwa kuiondowa Cameroon kutoka michuanio hii kwa kuifunga bao moja kwa bila na hivyo kuingia katika duru ya robo finali itakayoanza siku ya Jumamosi.

Matokeo haya yalitazamiwa, na wachambuzi wengi na mashabiki wa soka la Afrika, kutokana na kwamba ilikua ni mara ya kwanza kwa finali ya Kombe la Maaifa ya Afrika kuwepo na matokeo magumu ambapo hakuna timu iliyoweza kusonga mbele baada ya awamu mbili za mwanzo za duru ya makundi.

Mbali na matokeo hayo CAF iliamua kuhamisha mahala michunao ya robo finali itakapofanyika kutoka Monogomo na Ebebiyin, Hadoi Bata na Malabo, kutokana na kwamba imekuwa vigumu kucheza kwenye viwanja hivyo na hali ya majani yaliooteshwa wiki mbili tu kabla ya kuanza mashindano ya kombe hili.

Kubadilishwa huko kumewasababisha wafanya biashara wadogo dogo walokuwa wamejitayarisha na kuajirisha vibanda karibu na viwanja hivyo vya mpira kulalamika, wakidai kwamba watapata hasara kubwa.

Mfanya biashara mwoja anaeuza Shawarma Ahmadu ameimbia Sauti ya Amerika kwamba wamelipishwa dola 200 za kimarekani kwa siku tatu, hiyo ikiwa ni fedha nyingi kwa wafanyabiahsara hao pamoja na ukweli kamba tayari wamenunua bidhaa walotarajia kuuza.

Robo finali mbili za kwanza zitafanyika Jumamosi kati ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Kongo mjini Bata na Tunisia itapambana na wenyeji Equatorial Guinea mjini Malabo.

Robo ya pili itafanyika Jumapili tukisubiri matokeo ya bahati nasibu

XS
SM
MD
LG