Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 09:12

Tanzania na tuhuma za rushwa: Sakata la Escrow


Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete

Baada ya Tanzania kupitia kashfa kadhaa kama vile EPA, Richmond, Pembe za ndovu, Operesheni Tokomeza ni wachache waliodhania kama kuna kashfa nyingine itakayoitikisa nchi na kuendelea kutia doa utawala wa Rais Jakaya Kikwete.

Ni mgawanyo wa fedha zilizotajwa kuwa ni shilingi Bilioni 306, katika Akaunti ya Tegeta Escrow iliyopo Benki Kuu ya Tanzania ambao ulidaiwa kuhusisha vigogo wa serikali, majaji, viongozi wa dini, na wafanyabiasha waliopokewa fedha hizo ambazo wengine walida ni fedha za umma wakati baadhi ya wahusika wakisema hazikuwa fedha za serikali.

Ikiwa ni moja ya kashfa kubwa kwa serikali ya awamu ya nne, chimbuko la Escrow hasa ni nini? Akiwasilisha hoja ya kufichua kadhia hiyo, David Kafulila alisema baadhi ya maafisa wa ngazi za juu serikali walihusika katika ushawishi wa kuchotwa kwa fedha za akaunti ya Tegeta Escrow, na kumfanya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Benno Ndulu kuwa hana la kufanya kuzuia fedha kuchukuliwa.

Sakata hili likazidi kupamba moto na ukweli wa mambo uliaanza kufichuka kwa hatua kwa hatua. Bunge liliipa kamati ya bunge ya kudumu ya hesabu za serikali, kupitia ripoti ya uchunguzi uliofanywa na mkaguzi mkuu wa serikali, CAG ili kuwasilisha taarifa itakayo toa ukweli wa sakata hili.

Kamati hiyo na Bunge ikatoa mapendekezo manane ambayo yalimtaka, Rais Jakaya Kikwete ayafanyie maamuzi.

Mapendekezo hayo ni kuchukuliwa hatua vyombo vya uchunguzi kama Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa-Takukuru, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama. Lakini yaliyosuburiwa kwa hamu ni kuwajibishwa kwa watumishi wa serikali waliotajwa kushiriki katika kadhia hiyo, wakiwemo viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na wale wote waliotajwa kuhusika kuchota fedha hizo akiwemo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anna Tibaijuka.

Katika hotuba yake kwa taifa Disemba 22, 2014 ndipo Rais Kikwete alipotangaza uamuzi wa kumwachisha kazi Professa Tibaijuka kutokana na kile alichosema ni mgongano wa kimaslahi katika swala zima la akaunti hiyo ya Escrow. Rais Kikwete aliahidi kuwa uchunguzi unaendelea na hatua nyingine zitafuata.

XS
SM
MD
LG