Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 10:44

Dikteta wa zamani wa Haiti 'Baby Doc' Duvalier afariki


Dikteta wa zamani wa Haiti Jean-Claude 'Baby Doc' Duvalier, kushoto, awapungia mkono wafuasi wake kutoka baraza ya chumba cha hotel, Port-au-Prince, baada ya kurudinyumbani kutoka uhamishoni 2011.
Dikteta wa zamani wa Haiti Jean-Claude 'Baby Doc' Duvalier, kushoto, awapungia mkono wafuasi wake kutoka baraza ya chumba cha hotel, Port-au-Prince, baada ya kurudinyumbani kutoka uhamishoni 2011.

Kiongozi wa zamani wa utawala wa kimabavu wa Haiti, Jean Claude 'Baby Doc' Duvalier, amefariki kutokana na mshtuko wa moyo, akiwa na umri wa miaka 63.

Duvalier alitawala taifa hilo maskini la bahari ya Caribean kuanzia 1971 hadi kupinduliwa kwake na wananchi 1986.

Kama babake, 'Papa Doc' Duvalier, Baby Doc alitawala kwa ukatili akitumia hasa kikosi maalum cha polisi wanamgambo maarufu kwa jina la 'Tonton Macoutes', katika kuwakandamiza wananchi. Wanamgambo hao wanatuhumiwa kwa mauwaji na kutoweka kwa mamia ya watu kisiwani humo.

Baada ya kuishi miaka 25 uhamishoni Ufaransa, Baby Doc alirudi nyumbani 2011 kufuatia tetemeko kubwa kabisa la ardhi kuwahi kutokea nchini humo 2010.

Aliporudi nyumbani alifunguliwa mashtaka ya ulaji rushwa, utumiaji mbaya wa utawala wake pamoja na ukatili ulotendeka chini ya enzi yake.

XS
SM
MD
LG