Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:43

Ukraine yadai msafara wa misaada ya Russia ni uvamizi.


Mlinzi wa mpakani wa Russia akifungua lango la mpakani kwa magari ya kwanza ya Russia kuingia mashariki mwa Ukraine.
Mlinzi wa mpakani wa Russia akifungua lango la mpakani kwa magari ya kwanza ya Russia kuingia mashariki mwa Ukraine.

Ukraine inailaumu Russia kwa kuingilia nchi hiyo wazi wazi kwenye mpaka wao wa mashariki baada ya magari ya msafara wa misaada ya Russia kuanza kuingia nchini humo bila kukaguliwa na maafisa wa Ukraine.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine imetoa taarifa Ijumaa baada ya msafara wa magari 200 kuanza kuvuka mpaka baada ya siku kadhaa za kusubiri kwenye mpaka wa Ukraine ili kukaguliwa na maafisa wa Ukraine.

Moscow ilisema Ijumaa kwamba imechoshwa na kungoja ruhusa ya Kyiv kuendelea na safari . Dazeni ya magari makubwa yameripotiwa kuingia Ukraine Ijumaa huku yakiwa na mizigo ya chakula , maji , majenereta na magodoro.

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu imesema haitasindikiza msafara huo ndani ya Ukraine kwa sababu haijapata uhakika wa usalama.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema katika taarifa yake kwamba imejaribu kila njia mpaka imeshindikana na sasa msafara huo unaelekea mashariki mwa Ukraine kwenye ngome kuu ya waasi ya Luhansk , ambapo wakazi wanaishi kwenye eneo la vita kwa wiki kadhaa wakati waasi wanaounga mkono Russia wakiwa katika hali ngumu dhidi ya mapambano yao na majeshi ya serikali.

XS
SM
MD
LG