Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 11:00

Papa Francis awaalika viongozi wa Palestina na Israel Vatikan.

 Rais wa Israel Shimon Peres na waziri mkuu Benjamin Netanyahu wakiwa na Papa Francis katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ben Gurion karibu na Tel Aviv, May 25, 2014.
Rais wa Israel Shimon Peres na waziri mkuu Benjamin Netanyahu wakiwa na Papa Francis katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ben Gurion karibu na Tel Aviv, May 25, 2014.
Rais wa Israel Shimon Peres na mwenzake wa wapalestina Mahmoud Abbas wamekubali mwaliko wa Papa Francis waende Vatikan na kuomba Amani pamoja naye.

Akizungumza awali katika mji wa ukingo wa magharibi wa Bethlehem Papa Francis amesema muda umefika kwa kila mmoja kutafuta ujasiri wa kuwa mkarimu na kubuni njia katika kumaliza mzozo wa muda mrefu ambao umetonesha vidonda vingi sana . Aliwaalika marais hao wawili kwenda Vatikan kuombea Amani.

Papa Francis alilakiwa mjini Tel Aviv na rais wa Israel Shimon Peres na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kabla ya kusafiri kwenda Jerusalem.
XS
SM
MD
LG