Chama tawala cha Afrika Kusini kimeahirisha uchunguzi wa bunge wa shutuma za rushwa dhidi ya rais Jacob Zuma.Chama cha ANC kinasema hakina muda wa kuangalia suala hilo kabla ya uchaguzi ambao unafanyika chini ya siku 10 zijazo.
Ikiwa ni wiki sita baada ya maafisa wa juu wa kupambana na rushwa wa Afrika Kusini kutoa ripoti ya kurasa 400 ikieleza jinsi gani Bw.Zuma alivyotumia dola milioni 23 za umma kufanya matengenezo kwenye nyumba yake binafsi lakini kamati ya uchunguzi ambayo ilikutana mara mbili tu ilisimamisha uchunguzi huo.
Sababu ikiwa hakuna muda wa kutosha kabla ya uchaguzi. Cryil Ramaphosa ambaye ndiye makamu wa Bw.Zuma katika chama tawala cha ANC atakuwa makamu rais wa taifa hilo kama ANC ikishinda katika uchaguzi wa Mei 7 kama inavyotarajiwa.
Ramaphosa ametupilia mbali madai ya upinzani kwamba hii ni kukwepa kisiasa.