Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 00:24

Uhuru Kenyatta atembelea Mombasa.


Uhuru Kenyatta akipunga mkono mara baada ya kushinda katika uchaguzi wa Kenya.
Uhuru Kenyatta akipunga mkono mara baada ya kushinda katika uchaguzi wa Kenya.
Wanasiasa wakuu nchini Kenya Raila Odinga na mpinzani wake rais mteule Uhuru Kenyatta Jumatatu walizuru katika mji wa Mombasa, katika halfa tofauti.

Wiki moja baada ya kutangazwa mshindi, rais meule Uhuru Kenyatta amezuru Mombasa pamoja na familia yake kwa mapumziko ya mwishoni mwa juma.

Ziara hiyo ni kumbu-kumbu ya jinsi baba yake hayati Mzee Jomo Kenyatta alivyozuru sehemu hiyo, katika kipindi cha utawala wake akiwa rais wa Kenya kwa miaka 15.

Baadaye alipohutubia mamia ya waumini katika kanisa moja mjini Mombasa, Uhuru Kenyatta ametoa wito wa amani kwa Wakenya, akiwasihi wakatae kugawanywa katika misingi ya kikabila.

Uhuru atembelea Mombasa - 3:02
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:02 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Rais huyo mteule anawataka wananchi kuwa na utulivu wakati taifa linaposubiri uamuzi wa mahakama ya juu, kuhusu kesi iliyowasilishwa na wapinzani wake, kupinga ushindi wake kama rais wa nne wa Kenya.

Ziara ya Bwana Kenyatta katika eneo hilo la Pwani inaonekana kupangwa na muungano wa Jubilee, kwa sababu aliandamana na wafuasi wa muungano huo akiwemo seneta mteule wa County ya Nairobi Mike Mbuvi maarufu kama “Sonko”.

Wakati huo huo Sheikh Juma Ngao –mwenyekiti wa shirika la ushauri wa Kiislamu –KEMNAC, amejitokeza kuitetea tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya –IEBC, kutokana na lawama ilizolimbikiziwa katika uchaguzi huo mkuu, hasa wa urais.
Waziri mkuu Raila Odinga –aliye kinara wa muungano wa CORD naye amezuru Mombasa jumatatu kukutana na wafuasi wake.

Ameelezea matumaini ya kushinda kesi inayopinga ushindi wa Uhuru Kenyatta, huku akiwasihi wafuasi wake kuwa watulivu hadi pale kesi hiyo itakapo-kamilika.
XS
SM
MD
LG