Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 04:10

Uhuru Kenyatta aibuka mshindi wa urais Kenya.


Uhuru Kenyatta mshindi wa kiti cha Rais Kenya.
Uhuru Kenyatta mshindi wa kiti cha Rais Kenya.
Tume ya uchaguzi nchini Kenya imemtangaza rasmi Uhuru Kenya kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika nchini humo jumatatu.

Mwenyekiti wa tume hiyo Issack Hassan alisema Jumamosi kwamba Kenyatta alipata asilimia 50.7 ya kura zinazotosha kuepuka uchaguzi wa marudio.

Muda mfupi baada ya kutangazwa kwa Kenyatta kama mshindi mpinzani wake mkuu Waziri Mkuu Raila Odinga aliyeshika nafasi ya pili kwa asilimia 43 alitokea mbele ya mamia ya waandishi wa habari na kusema kuwa anapinga matokeo hayo na kwamba atafikisha malalamiko yake katika mahakama kuu ya Kenya. Odinga anadai kuwa tume ya uchaguzi ilifanya makosa kadha katika hesabu ya kura na orodha za wapigaji kura hasa katika maeneo ngome ya Odinga.

Odinga aliwataka wafuasi wake na Wakenya kwa jumla kuwa watulivu na kuacha mkondo wa sheria ufanye kazi yake.

Alhamisi mgombea mwenza wa Odinga, Kalonzo Musyoka alisema baadhi ya matokeo ya kura yamebadilishwa shutuma ambazo zilipingwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi.

Upande wa Odinga una muda wa siku saba kuwasilisha malalamiko yake mahakamani na mahakama itakuwa na muda wa wiki mbili kufanya uamuzi.

Endapo ushindi wa Kenyatta utasimama basi ataapishwa kuchukua madaraka Marchi 26.
XS
SM
MD
LG