Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 04:16

Cord wataka zoezi la kuhesabu kura lisimamishwe.


Kalonzo Musyoka, makamu rais wa sasa na mgombea mwenza wa Raila Odinga, akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari. Mar. 7, 2013.
Kalonzo Musyoka, makamu rais wa sasa na mgombea mwenza wa Raila Odinga, akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari. Mar. 7, 2013.
Mkuu wa tume ya uchaguzi Kenya anakanusha shutuma kwamba matokeo ya uchaguzi wa Jumatatu yanabadilishwa.

Katika mkutano kwenye makao makuu ya kituo cha kuhesabu kura Ahmed Isaack Hassan amesema kwasababu ya hatua kali ya kuthibitisha iliyopo “ hakuna nafasi ya aina yeyote ya kuweza kubadilisha matokeo.”

Hassan mkuu wa tume ya uchaguzi Kenya aliongea alhamisi baada ya mgombea mwenza wa Raila Odinga kusema kwamba kuhesabu kura kusimamishwe. Kalonzo Musyoka alisema kwamba wizi wa kura unaendelea.

Hassan alisema tume hiyo haiwezi kusimamisha kuhesabu kura . Alisema kama mtu yeyote akipinga matokeo anaweza kutumia njia ya kisheria iliyotolewa na katiba mpya ya Kenya.
XS
SM
MD
LG