Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 19:51

Rais Obama aapishwa rasmi.


President Barack Obama is officially sworn-in by Chief Justice John Roberts in the Blue Room of the White House during the 57th Presidential Inauguration in Washington, D.C., January 20, 2013. Next to Obama are first lady Michelle Obama, holding the Robin
President Barack Obama is officially sworn-in by Chief Justice John Roberts in the Blue Room of the White House during the 57th Presidential Inauguration in Washington, D.C., January 20, 2013. Next to Obama are first lady Michelle Obama, holding the Robin
Rais wa Marekani Barack Obama ataapishwa tena Jumatatu hadharani katika sherehe zitakazohudhuriwa na maelfu kwa maelfu ya watu upande wa magharibi mwa jengo la bunge ambako pia atatoa hotuba kabla ya kushiriki kwenye gwaride kuadhimishwa mwanzo wa muhula wa pili.

Takriban watu laki nane wanatarajiwa kukusanyika katika uwanja mkubwa wa – National Mall kushuhudia tukio hilo la kihistoria. Hii ni idadi ndogo ikilinganishwa na kipindi cha kwanza cha kuapishwa kwake ambapo takriban watu milioni mbili walihudhuria kuapishwa kwa rais wa kwanza mweusi nchini Marekani.

Bwana Obama aliapishwa kisheria Jumapili ikulu kwa sababu katiba inataka rais kuapishwa Januari 20. Jaji mkuu John Roberts aliongoza taratibu za kuapishwa kwa rais kama alivyofanya mwaka 2009.

Jumatatu katika tukio la kuapishwa bwana Obama atatumia biblia mbili za kihistoria, moja iliyomilikiwa na rais wa karne ya 19 Abraham Lincoln na nyingine ya mwanaharakati wa haki za kiraia Martin Luther King Jr., aliyeuwawa mwaka 1968.

Sherehe za kuapishwa kwa rais Obama zimekutana na maadhimisho ya sikukuu ya kuzaliwa kwa Martin Luther King Jr.
XS
SM
MD
LG