Wapiganaji wa kundi la waasi la M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congolwamechukua udhibiti wa mji wa Goma, risasi na mizinga ilirindima kwenye mji huo tangu jana usiku ambapo serikali ya DRC ilidai bado inaudhibiti wa mji wa Goma.
Lakini mwandishi wa VOA aliyeko Goma anaripoti kuwa askari wa jeshi la serikali FARDC wameukimbia mji huo na waasi wameukamata mpaka uwanja wa ndege wa Goma na hivi sasa mji uko chini ya udhibiti wa waasi hao.
Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani tayari watu 60,000 wameshapoteza makazi yao na wengi wanakimbilia Bukavu.
Hata hivyo Jumanne wafanya kazi wa Umoja wa Mataifa MONUSCO na viongozi wa serikali ya Congo walibebwa kwa ndege za UN na kupelekwa Bukavu na wengine Kinshasa. Jeshi la kulinda amani la umoja wa mataifa limeonekana katika mji likiwa katika vifaru vyao.
Waasi wanashikilia kwa sasa radio ya serikali na Uwanja wa ndege pamoja na mipaka ya Rwanda na DRC.