Rais wa Kenya William Ruto ametangaza Ijumaa wiki hii kuwa siku kuu ya kitaifa kuomboleza vifo vya watu 238 waliofariki kutokana na mafuriko.
Serikali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda zimetangaza kujenga upya ushirikiano wao wa kijeshi, kufuatia mkutano wa viongozi wakuu wa majeshi ya nchi hizo mbili uliofanyika katika mji wa Kasindi kwenye mpaka kati ya Congo na Uganda
Mwaka huu Sherehe za Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi zina hisia ya dharura ya kujitolea upya kwa haki za kijamii, wakati tunapopitia kipindi kigumu, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko ya haraka katika sehemu za kazi kutokana na maendeleo ya teknolojia.
Wabunge wanane wa Uganda wako Nairobi Kenya kwa ziara ya mafunzo juu ya kushughulikia changamoto za ukuaji wa miji nchini humo ikiwemo udhibiti makazi duni na kupitisha sera mahiri za ukuaji wa miji mikubwa.
China imemwalika waziri wa nishati wa Uganda mjini Beijing kujadili kuhusu bomba la mafuta ghafi la dola bilioni 5 la nchi hiyo ofisi ya rais wa Uganda ilisema Ijumaa.
Uganda inakabiliwa na upungufu mkubwa wa idadi ya simba kufuatia kupungua kwa asilimia 45 kwa wanyama hao katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, wizara ya utalii na wanyamapori ilisema Jumanne.
Mahakama ya Uganda Jumanne ilitupilia mbali rufaa ya kundi la kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja lililotaka usajili wa serikali, na kuamua kwamba kundi hilo lina lengo la kuendeleza shughuli “haramu”.
Serikali ya Haiti iliomba rasmi msaada wa usalama kutoka kwa nchi zote kote duniani, zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Mzozo wa Israel na wanamgambo wa Hamas ulitawala katika hotuba za viongozi wa nchi wanachama wa mataifa yasiyofungamana na upande wowote yaani Non-Aligned Movement (NAM) katika kongamano la 19 la Vuguvugu hilo lililofanyika Kampala, Uganda.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na mgombea wa zamani wa urais Bobi Wine leo Alhamisi amesema polisi waliizingira nyumba yake na kumuweka “chini ya kizuizi cha nyumbani” kabla ya maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika.
Mwili wa mwanariadha Benjamin Kiplagat ulipatikana ndani ya gari Jumamosi usiku kwenye viunga vya Rift Valley katika mji wa Eldoret nchini Kenya
Jeshi la Uganda limesema limemuua kamanda wa kikosi cha kundi la waasi la Islamist rebel Allied Democratic Forces (ADF) wanaoshutumiwa kufanya mauaji mabaya ikiwemo mauaji katika shule ya bweni.
Pandisha zaidi