Idadi kubwa ya wapiga kura vijana katika uchaguzi wa rais Marekani wanasema wanatamani wangekuwa na mtu mwingine na siyo Joe Biden au Donald Trump kumchagua.
Jimbo la Florida, hapa Marekani, limepitisha sheria mpya inayopiga marufuku utoaji mimba, baada ya wiki sita za ujauzito.
Wamarekani wenye asili ya Asia ni kundi ambalo linakua kwa haraka sana lenye wapiga kura wanaostahiki nchini Marekani, kwa mujibu wa kituo cha utafiti cha Pew.
Utani wa Rais wa Marekani Joe Biden ulipokelewa vyema na wale waliohudhuria chakula cha jioni cha waandishi huko White House Jumamosi usiku hapa Washington DC.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema mwaka 2024 ni mwaka wa uchaguzi usio wa kawaida wa kuangazia hatari kwa habari potofu na za uongo katika mitandao kwenye Mkutano wa demekrasia unaofanyika mjini Seoul leo.
Wakati wapiga kura wa Marekani wanajitayarisha kwa duru nyingine ya chaguzi za awali siku ya Jumanne, Rais wa Marekani, Joe Biden na mpinzani wake wa kisiasa Mrepublican Donald Trump walisafiri mwishoni mwa wiki kwenda kwenye majimbo ambayo matokeo yanaweza kwenda upande wowote.
Rais wa Marekani Joe Biden alitumia hotuba yake ya Hali ya Taifa Alhamisi usiku kama jukwaa la kuwarai Wamarekani kumchagua kwa muhula wa pili, huku akimkosoa vikali mpinzani wake mkuu, mgombea wa chama cha Republikan, Donald Trump.