Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 11, 2024 Local time: 06:28

Rostam Aziz ajiuzulu ubunge wa CCM


baadhi ya wafuasi wa chama cha CCM wakifurahia jambo katika mkutano
baadhi ya wafuasi wa chama cha CCM wakifurahia jambo katika mkutano

Anasema tuhuma dhidi yake na baadhi ya viongozi wengine wa CCM ni miongoni mwa sababu zilizomfanya achukue uamuzi huo

Jimbo la Igunga mkoani Tabora limepata pigo baada ya mbunge wake wa siku nyingi kupitia Chama Cha Mapinduzi -CCM Rostam Aziz, kutangaza rasmi kuacha nafasi ya ubunge wa jimbo hilo pamoja na kujivua nyadhifa zake katika chama ikiwa ni pamoja na ujumbe wa kamati ya Halmashauri Kuu ya chama -NEC.

Aziz alitangaza uamuzi huo Jumatano katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora kufuatia mkutano wa ndani wa chama cha CCM .

Katiba hotuba yake ya kujiuzulu Aziz alisema moja ya sababu za kuchukua uamuzi huo mgumu ni kutokana na tuhuma za ufisadi na madai ya kusababisha CCM kufanya vibaya katika baadhi ya majimbo katika uchaguzi mkuu uliopita.

Alisema tangu alipoanza kuwakilisha wilaya ya Igunga bungeni mwaka 1994 amekuwa muaminifu na mtu mwenye kujali maendeleo ya wananchi badala yake binafsi.

Lakini uamuzi huo umepokelewa kwa mtazamo tofauti na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa akiwemo Prf. Mwesiga Baregu ambaye amesema unaweza ikawa ni sehemu ya mabadiliko yanayoanza kujitokeza ndani ya CCM.

Aidha Prof. Baregu amesema wapo viongozi wengine walioanza kufanya taratibu za kuonesha nia ya kutaka kugombea urais mwaka 2015 hivyo haitashangaza kuona kwamba Rostam Aziz ni mmoja wao.

XS
SM
MD
LG