Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 10, 2024 Local time: 08:14

Uturuki, Iran na Morocco zinawania uchumi na jeshi ukanda wa Sahel


Ramani ikionyesha mataifa katika ukanda wa Sahel
Ramani ikionyesha mataifa katika ukanda wa Sahel

Vifaa vya kijeshi vya Uturuki, miradi ya maendeleo na miundombinu ya Morocco na Iran inazivutia serikali za kijeshi za Sahel

Uturuki, Iran na Morocco zinawania nafasi kubwa zaidi ya kiuchumi na kijeshi katika ukanda wa Sahel barani Afrika baada ya mtawala wa zamani wa kikoloni Ufaransa kulazimishwa kujiondoa kutoka eneo hilo tete.

Vifaa vya kijeshi vya Uturuki na miradi ya maendeleo na miundombinu ya Morocco na Iran inazivutia serikali za kijeshi za Sahel zenye matatizo ya kifedha kutokana na kukabiliwa na vurugu za jihadi.

Mali, Burkina Faso na Niger zimepitia mapinduzi tangu mwaka 2020, dhidi ya uasi wa kijihadi wa umwagaji damu. Watawala wao wa kijeshi tangu wakati huo wameondoka katika jumuiya pana ya Afrika Magharibi na kuunda makubaliano ya pamoja ya ulinzi ili kupambana na wapiganaji wa wanajihadi.

Forum

XS
SM
MD
LG