Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 06:16

Tanzania yazindua mtambo mpya wa kuzalisha umeme


Nyaya za umeme zinazosambaza umeme kwenye gridi ya kitaifa ya Tanzania.
Nyaya za umeme zinazosambaza umeme kwenye gridi ya kitaifa ya Tanzania.

Tanzania imezindua mtambo wa kwanza kwenye kinu kipya cha kuzalisha umeme wa maji ambacho kimepata upinzani mkali kutoka kwa wanamazingira kutokana na kuwa kimejengwa kwenye eneo lililoorodheshwa na Umoja wa Mataifa kama turathi ya Dunia.

Waziri wa Nishati na pia naibu waziri mkuu Doto Biteko, Jumapili wakati akitembelea kiwanda hicho cha Julius Nyerere chenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 alisema kwamba mtambo uliozinduliwa utaongeza megawati 235 za umeme.

Amesema kwamba uhaba wa umeme ulioshuhudiwa kwa miezi kadha utapungua baada ya kuzinduliwa kwa mtambo wa pili kwenye kiwanda hicho chenye jumla ya mitambo 9, mwezi ujao. Kabla ya kuanza kujengwa kwa mradi huo 2019, wanamazingira walionya kuwa kujengwa kwa bwawa kungeathiri mto muhimu unaopitia kwenye mbuga ya wanyama ya Selous.

Forum

XS
SM
MD
LG