Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 08:23

Serikali ya Uganda imelaani uamuzi wa Marekani kuongeza marufuku vibali vya usafiri na visa kwa maafisa wake


Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken akihutubia katika Sherehe ya Kuadhimisha Tafrija ya Muungano wa Uongozi wa Kimataifa wa Marekani (USGLC), Jumanne, Desemba 5, 2023, mjini Washington. (Picha ya AP/Mark Schifelbein).
Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken akihutubia katika Sherehe ya Kuadhimisha Tafrija ya Muungano wa Uongozi wa Kimataifa wa Marekani (USGLC), Jumanne, Desemba 5, 2023, mjini Washington. (Picha ya AP/Mark Schifelbein).

Serikali ya Uganda Jumatano imelaani uwamuzi wa Marekani kuongeza marufuku vibali vya usafiri, visa kwa maafisa wake ikiituhumu Washington kwa kulazimisha ajenda ya wapenzi wa jinsia moja LGBT barani Afrika.

Marufuku ya kusafiri ilitangazwa Jumatatu na kuwalenga maafisa ambao hawakutajwa ambao Marekani inahisi wanawajibika katika kuhujumu demokrasia na kukandamiza watu wa tabaka la wachache nchini Uganda, ikiwa ni pamoja na jamii ya LGBT. Uganda ilipitisha moja wapo ya sheria kali kabisa duniani dhidi ya wapenzi wa jinsia moja mwezi Mei ambayo inahitaji adhabu ya kifo miongoni mwa mambo mengine, kwa vitendo vya ushoga.

Waziri wa mambo ya nje wa Uganda Okello Oryem ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba kuna njama ya mapinduzi inayofanywa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani, ambayo anasema inaongozwa na watu wanaohimiza ajenda ya jamii ya LGBT Afrika.

Oryem anahoji, “kwanini wasipitishe vikwazo kama hivyo katika nchi za Mashariki ya Kati ambazo zina sheria sawa au hata kali dhidi ya LGBT? “Ikiwa wanakata kuwapiatia visa wabunge wetu, basi watakwenda Shangai, Guangzhou, na kuna maeneo mengine mengi mazuri kutembelea”

Marekani iliweka duru ya kwanza ya marufuku kwa maafisa wa Uganda kujibu sheria mwezi June na Benki Kuu ya Dunia ilisitisha mikopo kwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki mwezi Ogusti.

Forum

XS
SM
MD
LG