Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 21, 2024 Local time: 00:55

Rais Cyril Ramaphosa aita uhaini tangazo la kampeni ya chama cha upinzani


Afisa wa polisi wa Afrika Kusini akiendesha baiskeli kupita bango la matangazo ya Rais wa Afrika Kusini na mgombea wa chama tawala cha African National Congress (ANC) Cyril Ramaphosa kando ya Barabara ya Nelson Mandela katika kitongoji cha Seshego, karibu na Polokwane.
Afisa wa polisi wa Afrika Kusini akiendesha baiskeli kupita bango la matangazo ya Rais wa Afrika Kusini na mgombea wa chama tawala cha African National Congress (ANC) Cyril Ramaphosa kando ya Barabara ya Nelson Mandela katika kitongoji cha Seshego, karibu na Polokwane.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alielezea kuwa ni uhaini kwa hatua ya tangazo la kampeni la chama cha upinzani ambalo linaonyesha bendera ya taifa inayowaka moto, huku uhasama kati ya vyama vya siasa ukiongezeka wiki tatu kabla ya uchaguzi mkuu.

Tangazo la kampeni lililotolewa siku ya Jumatatu na chama cha Democratic Alliance linatumia bendera inayowaka kama alama ya kile inachosema ni hatari kubwa ya chama tawala cha African National Congress kubakia madarakani katika muungano na vyama vya mrengo wa kushoto.

"Nadhani ni uhaini," Ramaphosa aliwaambia waandishi wa habari wakati wa ziara yake katika jimbo la Limpopo. "Ni kitendo cha kisiasa kibaya zaidi ambacho mtu yeyote anaweza kukitekeleza," alisema, akishutumu DA kwa kunajisi ishara ya umoja wa kitaifa.

DA iliyo rafiki kwa wafanyabiashara ilishika nafasi ya pili kwa ukubwa wa kura katika uchaguzi uliopita miaka mitano iliyopita. Uchaguzi wa mwaka huu wa Mei 29 una upinzani mkali, huku kura za maoni zikipendekeza ANC itapoteza wingi wake kwa mara ya kwanza tangu ilipoingia madarakani miaka 30 iliyopita mwishoni mwa ubaguzi wa rangi.

Forum

XS
SM
MD
LG