Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 06:09

Mchungaji Kenya atuhumiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia


Ndugu na marafiki wakisubiri taarifa za wapendwa wao kutoka katika msitu wa Shakahola, Kenya ambako miili ya watu 90 ilifukuliwa. Picha na asuyoshi CHIBA / AFP
Ndugu na marafiki wakisubiri taarifa za wapendwa wao kutoka katika msitu wa Shakahola, Kenya ambako miili ya watu 90 ilifukuliwa. Picha na asuyoshi CHIBA / AFP

Mchungaji mmoja nchini Kenya anachunguzwa baada ya madai kwamba yeye na wazee wengine wa kanisa waliwanyanyasa kingono wanawake na wasichana kadhaa, polisi walisema.

Kesi hiyo ilibainika baada ya kanisa linaloendeshwa na Daniel Mururu katika kaunti ya Meru, katikati mwa Kenya, kuchomwa moto na wakazi wenye hasira mwishoni mwa mwezi uliopita.

Mururu, wa Kanisa la Pentekoste la Afrika Mashariki nchini Kenya, pamoja na wazee wa kanisa na washemasi, wanatuhumiwa kwa vitendo vya udhalilishaji vikiwemo kuwavua nguo, kuwaacha wanawake uchi, kuwanyoa nywele sehemu zao za siri na kufanya nao ngono , kulingana na ripoti ya polisi ya Jumatatu.

Zaidi ya wanawake na wasichana saba wenye umri kati ya miaka 17 hadi 70 wanadaiwa walidhulumiwa, ikiwemo msichana wa shule mwenye umri wa miaka 17 ambaye alipata ujauzito, ripoti hiyo ilisema.

Polisi walisema uchunguzi wao wa awali ulibaini kwamba Mururu alikuwa "anaendesha dhehebu" ambalo liliwafanya wafuasi wake kuwa na msimamo mkali.

Wanachama wa kanisa hilo walishawishiwa kufanya "vitendo vya udhalilishaji" kwa hofu ya matokeo kama vile "magonjwa na utasa" ikiwa watakaidi maagizo ya mchungaji, ripoti ya polisi ilisema.

Kenya, yenye idadi kubwa ya waumini wa kikristo, imekuwa ikipambana kudhibiti makanisa na madhehebu yasiyo na uadilifu ambayo yanajihusisha na uhalifu.

Katika kesi ya kutisha iliyoushtua ulimwengu, kiongozi wa dhehebu la njaa la mwisho wa dunia alikamatwa mwezi Aprili mwaka jana baada ya miili kugundulika imezikwa katika makaburi ya watu wengi.

Waokoaji walitumia miezi mingi kutafuta eneo la vichaka mbali na mji wa Malindi ulioko pembeni mwa Bahari ya Hindi na sasa wamefukua jumla ya miili 448 kutoka kwenye makaburi .

Uchunguzi wa maiti ulionyesha kuwa waathirika wengi walifariki kwa njaa. Lakini wengine, wakiwemo watoto, walionekana kunyongwa, kupigwa au kukosa hewa.

Sakata la kutisha linaloitwa "mauaji ya msitu wa Shakahola" liliifanya serikali kutoa wito wa udhibiti mkali wa madhehebu nchini.

Tume iliyoanzishwa na Rais William Ruto kuchunguza vifo hivyo na kuchambua sheria zinazohusu mashirika ya kidini iliwasilisha ripoti yake mwezi Julai, ikitoa wito wa mfano wa usimamizi wa serikali.

Forum

XS
SM
MD
LG