Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 28, 2025 Local time: 05:32

Mahakama Kuu Tanzania yatoa amri ya muda Mbowe asikamatwe


Mwenyekiti Freeman Mbowe
Mwenyekiti Freeman Mbowe

Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa amri ya muda kuhusiana na kesi ya kikatiba ambayo imefunguliwa na Mwenyekiti wa chama cha Chadema na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Tanzania Freeman Mbowe.

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili VOA, Mwanasheria mkuu wa Chadema Tindu Lissu amesema kuwa jopo la mahakama kuu lenye majaji watatu wametoa maamuzi ya muda kuhusiana na shauri hilo.

Kesi hiyo imefunguliwa dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mkuu wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Camilias Wambura.

Lakini mahakama imesema kuwa polisi watakuwa na uwezo wa kumwita Mbowe kwa ajili ya mahojiano kama wanataka, lakini hawana ruhusa ya kumkamata.

Amefafanua kuwa zuio la muda maana yake ni kwamba polisi wanazuiliwa kumkamata Mwenyekiti mpaka maombi hayo yataposikilizwa.

“Tumeomba hawa wanaotaka kumkamata Mwenyekiti wazuiliwe na mahakama mpaka hapo shauri la msingi lililofunguliwa na Mbowe litakapo amuliwa,” amesema Lissu.

Ameongeza kuwa mahakama kuu imesema itasikiliza maombi hayo siku ya Ijumaa (Februari 23).

Mahakama pia imetoa ruhusa kwa mwenyekiti kurekebisha maombi yake mahakamani ili kumwingiza mwanasheria mkuu wa serikali katika mashauri haya, amesema Lissu.

Ameongeza kuwa pia “tunaweza kufanya marekebisho mengine madogo madogo ambayo tutaona yanafaa katika shauri hili.

XS
SM
MD
LG