Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 25, 2024 Local time: 11:25

Marekani yapeleka wanajeshi wa ziada huko Mashariki ya Kati


Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Jenerali Pat Ryder katika mkutano na waandishi wa habari jijini Washington, Septemba 17, 2024. Picha ya AP
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Jenerali Pat Ryder katika mkutano na waandishi wa habari jijini Washington, Septemba 17, 2024. Picha ya AP

Marekani imepeleka idadi ndogo ya wanajeshi wa ziada huko Mashariki ya Kati kufuatia ongezeko kubwa la ghasia kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon, msemaji wa wizara ya ulinzi Meja Jenerali Pat Ryder alisema Jumatatu.

Ryder hakutoa maelezo zaidi kuhusu idadi ya wanajeshi waliopelekwa huko au kuhusu kile watakachofanya.

Hata hivyo, afisa mkuu wa Marekani ameiambia VOA kwamba ni darzeni ya wanajeshi na kazi yao ya kwanza itakuwa kujianda katika kusaidia raia wa Marekani kuondoka, iwapo vita vitazuka katika kanda hiyo yote.

Afisa mwingine wa Marekani amesisitiza kwamba hali haijafikia kiwango ambapo usaidizi wa jeshi kuwaondoa raia wa Marekani unahitajika.

Ikibidi kuwaondoa watu, jeshi la Marekani lina wanajeshi waliopelekwa eneo la karibu na watatekeleza kazi hiyo, afisa mwingine ameiambia VOA. Wote waliomba majina yao yasitajwe.

Forum

XS
SM
MD
LG