Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 02:22

Mahakama ya Kenya yasitisha mpango wa kukodisha uwanja wa ndege wa JKIA


Picha ya maktaba ya wasafiri wakiwa wamekwama kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA, kufuatia mgomo wa muungano wa wafanyakazi.
Picha ya maktaba ya wasafiri wakiwa wamekwama kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA, kufuatia mgomo wa muungano wa wafanyakazi.

Mahakama ya Juu ya Kenya imesitisha kwa muda mkataba wa kukodishwa kuwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta – JKIA,  kwa muda wa miaka 30, kwa kampuni ya India ya Andani Group, kwa lengo la kuupanua.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, chama cha mawakili nchini, LSK, pamoja na shirika la kutetea haki za binadamu la Kenya Human Rights Commission, KHRC, wameiambia mahakama Jumatatu, kwamba Kenya inaweza kujipatia dola bilioni 1.85, zinazohitajika kukarabati uwanja huo jijini Nairobi, bila msaada kutoka nje.

Mashirika hayo yameiambia mahakama kwamba hatua hiyo ni yenye gharama kubwa, inatishia ajira za watu na wala haina faida yoyote kwa walipa kodi wa Kenya, kulingana na nyaraka zilizowasilishwa na KHRC. Kampuni ya Andani haijasema lolote kufuatia hatua hiyo, wakati msemaji wa idara ya kitaifa ya usafiri wa anga, aliiambia Reuters kwamba hawana maoni yoyote kwa kuwa suala hilo liko mahakamani.

Mwezi uliopita, muungano wa wafanyakazi kwenye uwanja huo ulitishia kuitisha mgomo kwa madai kwamba mkataba huo ungepelekea kupoteza ajira kwa wafanyakazi wa Kenya.

Forum

XS
SM
MD
LG