Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 03, 2024 Local time: 21:47

Mahakama ya Afrika kusini yaidhinisha Zuma kuendelea na nembo ya MK


Nembo ya chama kipya cha upinzani nchini Afrika kusini cha uMkhonto we Sizwe (MK). April 11, 2024.
Nembo ya chama kipya cha upinzani nchini Afrika kusini cha uMkhonto we Sizwe (MK). April 11, 2024.

Jina la MK lina upinzani linafanana na tawi la silaha la ANC ambalo Mandela aliliongoza enzi za ubaguzi wa rangi.

Mahakama nchini Afrika Kusini imeruhusu chama kipya kinachoungwa mkono na Rais wa zamani Jacob Zuma kutumia jina na nembo yake katika uchaguzi mkuu wa mwezi Mei, na kutupilia mbali madai ya chama tawala cha ANC ya wizi wa nembo za biashara.

Mahakama kuu ya Durban imetoa uamuzi wa kukipendelea chama cha uMkhonto we Sizwe (MK) katika msururu wa kesi za hivi karibuni kati ya Zuma na chama chake cha zamani cha siasa, chama tawala cha African National Congress (ANC).

Chama cha ANC kilijaribu kukizuia chama kipya cha kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 kutumia jina la MK kwa madai ya wizi wa haki miliki. Jina la MK lina upinzani kwa kuwa linafanana na lile la tawi la silaha la ANC ambalo Nelson Mandela aliliongoza kutoka uhamishoni wakati wa enzi za ubaguzi wa rangi.

Maombi hayo yanatupiliwa mbali kwa gharama, mamlaka ya mahakama ilisema katika uamuzi uliotolewa kwa njia ya televisheni.

Forum

XS
SM
MD
LG