Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 10:15

Jeshi la Sudan halitaki mpatanishi wa umoja wa mataifa


Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan akiwa pamoja na wanajeshi wake mjini Khartoum. May 30, 2023,
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan akiwa pamoja na wanajeshi wake mjini Khartoum. May 30, 2023,

Serikali ya Sudan imesema kwamba haitaki mjumbe maalum wa umoja wa mataifa nchini humo, ambaye ni mpatanishi mkuu katika mazungumzo ya kumaliza vita kati ya jeshi la Sudan na kundi la kijeshi la RSF.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Sudan inajiri wiki chache baada ya kiongozi wa jeshi la Sudan Generali Abdel Fattah Burhan, kutaka Volker Parthes kuondolewa majukumu yake ya kuwa mpatanishi katika mzozo huo.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres amefamishwa kuhusu uamuzi wa serikali ya Sudan.

Tangu pril 15, jeshi la Sudan, likiongozwa na Burhan limekuwa likipigana na kikosi maalum cha jeshi cha RSF kinachoongozwa na Generali Mohmmed Hamdaan Dagalo, kila upande ukilenga kupata nguvu za kuongoza serikali.

Zaidi ya watu 860 wamefariki kutokana na vita hivyo na muungano wa madaktari nchini Sudan umesema kwamba huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Forum

XS
SM
MD
LG