Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 03:49

ACT wazalendo Zazibar watishia kujiondoa kutoka serikali ya Umoja, GNU


Watu wakiwa katika foleni ya lupigia kura huko Zanzibar Octoba 28, 2020. Picha na Patrick Meinhardt / AFP.
Watu wakiwa katika foleni ya lupigia kura huko Zanzibar Octoba 28, 2020. Picha na Patrick Meinhardt / AFP.

Chama cha ACT Wazalendo, Zanzibar kinachounda serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) kimetishia kujiondoa kutoka muungano huo kutokana na baadhi ya makubaliano kushindwa kutekelezwa na rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Serikali ya umoja huo wa kitaifa (GNU) iliundwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 kufuatia ghasia zilizotokana na upinzani kutokubaliana na wa matokeo ya uchaguzi.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Makamu Mwenyekiti wa chama cha ACT wazalendo Zanzibar Ismail Jussa ameeleza nia ya chama hicho kujitoa kwenye serikali hiyo kutokana na baadhi ya makubaliano ya kuundwa kwa serikali hiyo kutotekelezwa na Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

“Tumechoka na ahadi zisizotekelezeka na kiongozi ambaye ameshindwa kusimamia kauli zake na maneno yake tumeamua kwamba sasa wakati umefika wa kupeleka ujumbe kwamba hatuwezi kuwa sehemu ya serikali ya umoja wa kitaifa wakati yale tuliyokubaliana kwamba yatekelezwe hayatekelezwi,” amesema Jusa.

Baadhi ya makubaliano ambayo mpaka sasa hayajatekelezwa ni pamoja na kuundwa kwa kamati ya uchunguzi kuchunguza matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi, kufanyika kwa marekebisho ya mfumo nzima wa uchaguzi, kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki pamoja na kuwepo kwa mfumo wa kudumu wa kuyadumisha maridhiano.

Dr Richard Mbunda Muhadhiri wa masuala ya siasa katika chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amesema maendeleo ya kisiasa yameweza kupatikana Zanzibar kutokana na maridhiano hayo, hivyo kuyaondosha maridhiano kutapelekea kurudisha nyuma maendeleo na machafuko ya kisiasa kujitokeza tena visiwani humo.

"Sasa tukirudi nyuma kwenye maridhiano ni dhahiri kwamba machafuko sasa yataanza kuonekana tena na labda pengine watu wataanza kuishi tena kwa uwoga maana siasa za Zanzibar zimejaa hujuma mtu hawezi kununua bidhaa ya mtu yule kwasababu labda pengine ya itikadi zake watu hawazikani watu hawaongei,” amesema Mbunda.

Hata hivyo kwa upande wa chama tawala cha CCM kupitia kwa Khamis Mbeto Khamis, katibu wa kamati maalumu ya halimashauri kuu ya taifa, idara ya itikadi uenezi na mafunzo Zanzibar, amesema madai ya Chama cha ACT Wazalendo hayapo katika katiba na hayakuwa makubaliano rasmi hivyo wanapaswa kutumia busara kutetea madai hayo.

“Kuna vitu wenzetu wanavidai inawezekana hivyo vitu vilizungumzwa lakini sisi tunasimamia katika misingi ya katiba na mabadiliko ya kumi ya katiba hivyo,” amesema Khamis

Aliomgeza kuwa “vitu vilivyotajwa havipo wala havikuandikwa popote ni matakwa ya mazungumzo kama ya Rais na nchi yoyote makini vitu huwekwa kwenye maandishi”

Dr. Ntui Ponsian Muhadhiri Biashara na Uchumi SAUT Mwanza amemalizia kwa kuvitaka vyama hivyo viwili kukaa katika meza ya mazungumzo na kumaliza tofauti zao kwa kuwa maridhiano ndio msingi wa maendeleo

Hii ripoti imetayarishwa na Amri Ramadhani, mwandishi wa VOA Dar es Salaam.

Forum

XS
SM
MD
LG