Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 09:24

Mtoto wa Museveni asema ameachana na mpango wake wa  kuwania urais


Lt. Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, alipo hudhuria hafla ya shukrani huko Entebbe, Uganda Jumamosi, Mei 7, 2022.
Lt. Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, alipo hudhuria hafla ya shukrani huko Entebbe, Uganda Jumamosi, Mei 7, 2022.

Mtoto wa kiongozi wa muda mrefu nchini Uganda Yoweri Museveni alisema  Jumamosi kuwa ameachana na mpango wake wa  kuwania urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2026, akiwataka wafuasi wake kumuunga mkono baba yake.

Rais Museveni ambaye ameiongoza nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa miaka 38, anatarajiwa kwa kiasi kikubwa kuwania tena kiti cha urais japokuwa bado hajathibitisha kugombea.

"Ningependa kutangaza kwamba sitakuwa kwenye karatasi ya kura 2026," alisema Muhoozi Kainerugaba katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Ninamuidhinisha kikamilifu Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi ujao," alisema, akiwasihi wafuasi wake kumuunga mkono baba yake kwa muhula wa saba.

Forum

XS
SM
MD
LG