Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:21

Nyamitwe akanusha hakuna ghasia Burundi


Willy Nyamitwe, mshauri mwandamizi wa Rais Pierre Nkurunziza.
Willy Nyamitwe, mshauri mwandamizi wa Rais Pierre Nkurunziza.

Mshauri mwandamizi kwa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, bwana Willy Nyamitwe aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba picha za ghasia ya maandamano, na kuchomwa kwa mali katika mji mkuu Bujumbura zinazotangazwa kote duniani si matukio ya hivi karibuni.

Bwana Nyamitwe alisema watu ambao wamekuwa wakifyatua risasi usiku na kuuwa watu wasio na hatia katika mji mkuu wameshindwa na kwamba hali katika mji mkuu imerudi kuwa ya kawaida. Alisema bado wanakabiliana na watu ambao wanaendelea kuuwa watu wasio na hatia ambao wanatoka upande wa upinzani.

Alisema watu ambao wamekamatwa na kusalimisha silaha zao wametoka upande wa upinzani. Aliongeza kwamba mauaji ya hivi karibuni ya maafisa watatu wa serikali yalikuwa vitendo vya ugaidi na walipanga kufanya hivyo kabla ya ujumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kutembelea nchini humo.

Nembo ya Umoja wa Mataifa-UN
Nembo ya Umoja wa Mataifa-UN

Wakati huo huo marais wawili wa zamani wa Burundi wamewasilisha maombi mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kulitaka baraza hilo kuihimiza serikali ya Bujumbura kukubali kupelekwa kwa kikosi cha kulinda amani kitakachongozwa na Umoja wa Afrika nchini humo.

Marais wa zamani Domitien Ndayizeye na Jean Baptiste Bagaza walikutana Alhamis na ujumbe wa baraza hilo unaotembelea Bujumbura kwa wakati huu kujaribu kuzuia ghasia za kisiasa ambazo zimeshawauwa takriban watu 439 tangu mwezi April mwaka jana.

XS
SM
MD
LG