Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:35

Makamanda wa al-Shabaab wauwawa Somalia


Wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab nchini Somalia
Wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab nchini Somalia

Shambulizi moja la ndege zisizotumia rubani yaani Drone kusini mwa Somalia liliuwa makamanda wawili wa jeshi kutoka kundi la wanamgambo wa al-Shabab lenye uhusiano na al-Qaida.

Shambulizi hilo lilitokea Jumatano jioni karibu na mji wa Bardere katika mkoa wa Gedo.

Mwandishi wa habari katika eneo aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba majina ya wanamgambo waliouwawa yalikuwa ni Jama Dere, naibu kamanda wa wapiganaji wa kundi la al-Shabab latika mkoa wa Lower Juba na Ismael Jabhad, ofisa mwandamizi wa jeshi kwa kundi la al-Shabaab.

Mji wa Bardere upo kilomita 400 kusini-magharibi ya Mogadishu ni ngome kuu ya kundi la al-Shabab. Majeshi ya serikali ya Somalia na majeshi ya Ethiopia wanajiandaa kwa shambulizi la kuuteka tena mji.

Vyombo vya habari vya Somalia vinaripoti kwamba ni ndege ya Marekani isiyotumia rubani ambayo ilifanya shambulizi lakini hakuna uthibitisho wowote kutoka jeshi la Marekani.

Mfano wa ndege ya Drone
Mfano wa ndege ya Drone

Marekani imefanya mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani kushambulia viongozi wa al-Shabaab siku za nyuma ikiwemo shambulizi kwa kiongozi mkuu wa kundi, Ahmed Abdi Godane ambaye aliuwawa mwezi Septemba mwaka 2014.

Kundi la al-Shabaab limeondolewa sehemu kubwa ya maeneo iliyokuwa ikiyadhibiti kukatisha kusini na kati kati ya Somalia. Lakini kundi linaendelea kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga kote nchini Somalia na Kenya ikiwemo shambulizi moja kwenye chuo kikuu cha garissa kilichopo Kenya hapo mwezi April ambapo watu 148 waliuwawa.

XS
SM
MD
LG