Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 22:37

Ethiopia kushambulia al-Shabab.


Mabaki ya jengo lililoshambuliwa na al-Shabab mjini Mogadishu
Mabaki ya jengo lililoshambuliwa na al-Shabab mjini Mogadishu

Mashahidi wanasema takriban wanajeshi 3,000 wa Ethiopia wameingia Somalia ikisemekana wana nia ya kushambulia wanamgambo wa al Shabab. Wakazi wa eneo la kusini magharibi la Gedo wamesema wanajeshi wenye vifaru na magari yenye silaha walianza kuvuka mpaka jumatatu na kuwa wameonekana kwenye mji wa Luq.

Awali, mamlaka ya eneo hilo yalikuwa yameambia VOA kuwa vikosi vilikuwa vinaandaliwa kwa mashambulizi kwenye maeneo yalio chini ya udhibiti wa al- Shabab ikiwemo ngome kuu ya mwisho ya mji wa Bardere.

Wanamgambo hao wamepoteza sehemu kubwa waliyokuwa wameshikilia huko Somalia lakini bado wanafanya mashambulizi makubwa. Jumanne shambulizi lililofanywa na al-Shabab kwenye makazi kaskazini mashariki mwa Kenya yaliwauwa watu 14.

XS
SM
MD
LG