Karibu watu 500 wameuliwa katika mashambulizi 150 tofauti kuanzia 2012 hadi 2015 kote nchini Kenya, hii ni kufuatana na ripoti iliyochapishwa Jumatano mjini Nairobi.
Kufuatana na takwimu za polisi, vifo vingi vimetokea Nairobi, Garissa na Mandera, pamoja na miji ya pwani ya Kenya. Kati ya Januari 2012 hadi Sisemba mwaka jana watu 113 waliuliwa mjini Nairobi huku watu 68 waliuliwa mjini Mandera.
Hapo April pili magaidi waliwauwa watu 148 katika Chuo Kikuu cha Garissa ikiwa ni idadi kubwa ya vifo kutokana na shambulizi moja.
Vifo hivyo vyote vinaripotiwa ni kutokana na mashmabulizi ya wanamgambo wa kundi la kisomali la Al- Shabab.
Takwimu hizo zimetolewa siku moja baada ya watu 14 kuuliwa katika mji wa Mandera na siku tano baada ya wafugaji kuuliwa na wanamgambo wa Al-Shabab katika