Wahubiri kote nchini Kenya Jumapili walitoa wito wa uchaguzi wa amani. Francis wambua, kutoka chama cha wakatoliki wanaume, amesema waumini wengi walifika makanisani na kusali kuomba amani na umoja wa kitaifa kabla ya upigaji kura wa Jumatatu asubuhi.
Muuza magazeti mmoja mjini Mombasa, Morris Oduor anasema hana wasi wasi kuhusu kurejewa kwa ghasia kama zile za uchaguzi uliopita.
Anasema ujumbe wa amani umejitokeza upo kila mahali ukilinganisha na mara ya mwisho ilivyokuwa. Anasema wakati ule kulikuwa na hotuba za chuki na kundi moja likilishutumu kundi jingine, lakini wakati huu kila mtu anahubiri amani, nadhani Kenya inatia moyo sana.
Mivutano bado kwa ujumla ni mikubwa, na baadhi ya maafisa polisi elfu 99 wamepelekwa kote nchini Kenya.
Rais anayeondoka mamlakani Mwai Kibaki na wagombea wote wa urais wameomba kuwepo na uchaguzi wa amani. Wagombea wawili wa mbele kwa mujibu wa kura za maoni, waziri mkuu Raila Odinga na makamu waziri mkuu Uhuru Kenyatta wote wameahidi kuheshimu matokeo ya kura.
Wapiga kura milioni 14 nchini Kenya wanatarajiwa kushiriki zoezi hilo hivi leo kwa ajili ya rais ajaye, bunge, magavana na maafisa wengine.