Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 17, 2024 Local time: 21:37

Polisi 30 wauwawa katika shambulizi la kushtukiza Kenya

View of South America and portions of North America and Africa from the Mercury Dual Imaging System’s wide-angle camera aboard MESSENGER (Mercury Surface, Space Environment, Geochemistry, and Ranging). (Credit: NASA/Johns Hopkins University Applied Physics Laboratory/Carnegie Institution of Washington)

Polisi wa Kenya wanasema kwamba takriban polisi 30 wameuwawa katika shambulizi la kushtukiza lililotokea katika wilaya ya Baragoi, kaunti ya Samburu, Kaskazini mwa nchi.

Msemaji wa polisi ya Kenya Eric Kiraithe anasema maafisa hao walishambuliwa Jumamosi wakati lori lao lililopita huko Baragoi. Anasema maiti 11 walipatikana hiyo hiyo Jumamosi na wengine 19 walipatikana siku ya pili. Watu 9 walonusurika wamelazwa hospitali.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:44 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Bw Kiraithe ameapa kwamba walofanya kitendo hicho watakamatwa. " Kumekuwa na watu kadhaa walokamatwa na uchunguzi unaendelea," alisema. "Wahalifu walotenda uhalifu huo watafikishwa mahakamani kwa njia yeyote ile.."

Hakuna aliyedai kuhusika na shambulio hilo. Polisi wanadhani ni wezi wa n'gombe ambao walihusika na shambulio jingine huko Baragoi mwezi uliyopita na kusababisha vifo vya watu 13.
XS
SM
MD
LG