Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 12, 2025 Local time: 02:00

Chama cha wanasheria Tanzania chataka tume ichunguze uhalali wa majaji walioteuliwa


Ramani ya Tanzania
Ramani ya Tanzania

Chama cha wanasheria Tanzania bara, Tanganyika Law Society kimetaka kuundwa kwa tume maalumu kwa ajili ya kuchunguza uhalali wa kuteuliwa kwa majaji kadhaa ambao uteuzi wao katika siku za hivi karibuni ulizua mjadala mkubwa ndani ya Bunge.

Rais wa chama hicho Bwana Fransis Stola amewaambia wanaandishi wa habari jijini Dare s as laam kuwa ili kuondoa kiwingu kinachoandama taasisi ya mahakama, rais wa Tanzania Jakaya Kikwete anapaswa kuuunda tume maalumu ambayo itakuwa na kazi ya kuchunguza uhalali wa majaji hao kama uteuzi wao ulivunja katiba ya Jamhuri vinginevyo wananchi wanaweza kuanza kukosa imani na chombo cha mahakama

Tahadhari na wanasheria hao inakuja siku chache tu baada ya makundi ya kisiasa kuzozana vikali ndani ya vikao vya Bunge wakilalamika kuwa uteuzi wa majaji kadhaa ulifanywa bila kuzingatia misingi inayopatikana ndani ya Katiba ya nchi.

Katika jambo la pili chama hicho kimelaani juu ya kile ilichokiita matumizi ya nguvu yanayofanywa na taasisi za dola dhidi ya wananchi, na akilitaja tukio la hivi karibuni la kuuliwa kwa mwandishi wa habari mmoja mkoani Iringa anayedaiwa kupigwa bomu na polisi, kuwa ni matukio yanayopaswa kukemewa na kulaaniwa.

Pamoja na hayo, chama hicho cha wanasheria kimeipinga kamati iliyoundwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchini kwa ajili ya kuchunguza mazingira yaliyosababisha kifo cha mwandishi huyo.

Kamati hiyo inayoundwa na wajumbe watano tayari imeanza kazi mkoani Iringa
XS
SM
MD
LG