Rais wa Marekani Donald Trump amesema Alhamisi kwamba hivi karibuni atazungumza na mwezake wa Russia Vladimir Putin ili kujaribu kumshinikiza amalize vita vilivyodumu kwa karibu miaka mitatu na jirani yake Ukraine.
Wabunge wa Marekani Alhamisi wamewasilisha msuada unaolenga kusitisha hadhi maalum ya kibiashara kwa China na Marekani, kuongeza ushuru kwa kiwango cha juu, pamoja na kumaliza sera ya kutolipiwa ushuru kwa bidhaa za thamani ndogo kutoka China.
Rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh amesema ana nia ya kuchukua tena udhibiti wa chama chake cha siasa na kutangaza kwamba “anarudi nyumbani”, katika ujumbe wa sauti ambao shirika la habari la AFP limeupata Alhamisi.
Moto mwingine wa nyika umejitokeza na kusambaa kwa kasi katika eneo moja kaskazini mwa Los Angeles Jumatano ukiongezeka kutokana na upepo mkali na hali ya ukavu.
Saratani ya tezi dume ni ugonjwa unaosumbua katika jamii nyingi hivi sasa ugonjwa ambao unaelezwa kwamba unatokana na sababu mbalimbali ikiwemo umri mkubwa au maambukizi ya mara kwa mara katika tezi dume ugonjwa ambao unawakabili wanaume hasa wanaofikia umri mkubwa.
Baraza la Mawaziri la Gabon lilisema Jumatano jioni kwamba uchaguzi wa rais utafanyika Aprili 12, mwaka huu
Waziri wa mambo ya nje wa India Subrah-manyam Jaishankar amesema New Delhi iko tayari kuwapokea raia wa India wasiokuwa na nyaraka halali nchini Marekani
Hata kabla ya kuwepo ofisini kwa saa 48, rais wa Marekani Donald Trump alituma ujumbe wa kukabiliana na China kwenye anga za juu, na kwamba utawala wake utakuwa na ajenda kubwa ifikapo kuendesha Marekani mbele kwenye teknolojia ya akili mnemba au AI pamoja na miundombimu inayoiendesha.
Mamlaka za California Jumatano zimetoa amri ya watu kuondoka kwenye maeneo ya ndani baada ya moto mpya kuzuka ukiwa na upepo mkali kwenye milima iliyopo kasakzini mwa Los Angeles.
Sudan Kusini Jumatano imeamuru kampuni zinazotoa huduma za intaneti kuzuia mitandao ya kijamii, ikiwemo Facebook na TitTok, kufuatia maandamano yenye vurugu yaliyochochewa na vifo vya raia wake wiki iliyopita.
Pentagon itaanza kupeleka hadi wanajeshi 1,500 ili kusaidia kulinda mpaka wa kusini na Mexico katika siku za karibuni.
Pandisha zaidi