Mtaalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, William O’Neil Jumanne ameambia wanahabari mjini New York kwamba hali ya kiusalama nchini humo ni tete huku akisihi wahusika wa kitaifa na kimataifa kuheshimu haki za binadamu.
Basi hilo lilibeba zaidi ya watu 50 waliokuwa wanakwenda kazini wakati lilipoanguka katika barabara yenye shughuli nyingi.
Mivutano kati ya Rais Salva Kiir na Makamu wake wa Kwanza wa Rais Riek Machar ikizusha hofu ya kurejea vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kundi la Al Shabaab limedai kuhusika na shambulio hilo katika taarifa yake na lilisema limewaua zaidi ya watu 10.
Sumy iko katika mpaka kutoka mkoa wa Kursk nchini Russia ambako vikosi vya Ukraine vilianzisha mashambulizi mwezi Agosti.
Wakati huo huo Rais wa Taiwan Lai Ching-te amesema ni watu wa Taiwan pekee wanaoweza kuamua mustakabali wao.
Papa Francis alifuatilia ufunguzi wa mkutano huo kwa njia ya video siku ya Jumapili.
Tukio limetokea saa chache baada ya wanajeshi wa Korea Kusini na Marekani kuanza mazoezi yao ya pamoja ya kila mwaka.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ambaye afya yake imeendelea kuimarika wakati akipokea matibabu kutokana na homa ya mapafu, Jumapili aliwashukuru madaktari pamoja na wahudumu wa afya, ingawa hakuweza kuongoza maombi ya Angelus kwa mara ya nne mfululizo.
Majeshi ya Wanamaji ya Iran, Russia na China yatafanya mazoezi ya katika pwani ya Iran wiki hii katika jitihada za kuimarisha ushirikiano, vyombo vya habari vya Iran vimeripoti Jumapili.
Pandisha zaidi