Rais wa Marekani, Joe Biden, Jumapili amemsamehe mzalendo mweusi Marcus Garvey, ambaye alimshawishi Malcolm X na viongozi wengine wa haki za kiraia ambaye alipatikana na hatia ya ulaghai wa barua katika miaka ya 1920.
Wizara ya fedha ya Marekani Alhamisi ilitangaza vikwazo dhidi ya Abdel Fattah al-Burhan, ikilituhumu jeshi lake kwa kushambulia shule masoko na hospitali pamoja na kutumia mtindo wa kuwanyima wananchi chakula kama silaha.
Waokoaji wa Afrika Kusini walikuwa wakifanya juhudi za mwisho siku ya Alhamisi kufahamu kama kuna mtu yeyote aliyenusurika kwenye machimbo haramu ya dhahabu
IOM inasema watu waliokoseshwa makaazi Haiti wameongezeka kufikia asilimia 87 kutokana na vurugu za makundi ya uhalifu.
Maafisa wa Ujerumani wamesema ziara hiyo inaihakikishia Ukraine kupata msaada katika vita vyake dhidi ya Russia
Mazungumzo hayo yanakuja baada ya miezi 15 ya mapigano huko Gaza na yanaelezewa kuleta mafanikio kwa wiki hii.
Bunge jipya la Msumbiji limekutana Jumatatu kwenye mji mkuu , ambapo wabunge 210 walikula viapo vyao huku vyama vya upinzani vikisusia na kuendelea na maandamano baada ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni.
Amekuwa kizuizini katika mji mkuu wa Kampala tangu alipokamatwa Novemba 2024 akiwa na msaidizi Obeid Lutale.
Rais wa zamani wa Nigeria Chifu Olusegun Obasanjo amefanya ibada ya ukumbusho huko Abeokuta kusini magharibi mwa Nigeria kwa heshima ya Rais zamani wa Marekani Jimmy Carter ambaye alifariki decemba 29 na kuzikwa wiki iliyopita.
Nayo wizara ya Ulinzi ya Russia imesema iliingilia kati na iliharibu ndege zisizokuwa na rubani 85 za Ukraine usiku wa kuamkia leo.
Msafara huo ulitoka kutoa pole ya msiba kwa mwenzao ulishambuliwa na majambazi msemaji wa polisi alisema.
Ni baada ya mivutano juu ya mipango ya Addis Ababa kujenga kambi ya jeshi la majini katika mkoa wa Somalia uliojitenga.
Pandisha zaidi