Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani yathibitisha raia wa Saudia na Marekani  amekamatwa Saudi Arabia

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Washington, Machi 10, 2022.(REUTERS)

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilithibitisha kwamba raia wa Saudia Arabia na Marekani amezuiliwa nchini Saudi Arabia, na kusema kwamba Washington imekuwa ikielezea wasiwasi wake mara kwa mara juu ya kufungwa kwake jela, hivi karibuni siku ya Jumatatu.

Saudi Arabia mwanzoni mwa Oktoba ilitoa hukumu ya kifungo cha miaka 16 jela kwa raia wa Saudia na Marekani Saad Ibrahim Almadi, gazeti la Washington Post liliripoti Jumatatu jioni, kutokana na ujumbe wake wa Twitter ulioikosoa serikali ya Saudia.

Almadi alishtakiwa kwa kuwa na itikadi ya kigaidi, kujaribu kuvuruga Ufalme, pamoja na kuunga mkono na kufadhili ugaidi, gazeti la Post liliripoti. Pia alipewa marufuku ya kusafiri ya miaka 16.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, naibu msemaji wa Idara Vedant Patel alithibitisha kukamatwa kwa Almadi na kusema Washington ilieleza wasiwasi wake kwa mara ya kwanza na Riyadh mnamo mwezi Desemba 2021, mara tu ilipofahamishwa kuhusu kukamatwa kwake.