Wanasheria na mashirika ya kutetea haki za binadamu yameishutumu Iran kwa kumnyongwa mwanamume anayetuhumiwa kuuwa Walinzi wa Mapinduzi wakati wa maandamano ya haki za wanawake.
Familia ya Gholamreza “Reza” Rasaei na wakili wake hawakufahamishwa mapema kuhusu mauaji hayo yaliyofanyika Jumatatu.
Tovuti ya mahakama ya Iran baadaye ilitangaza hatua yake dhidi ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye Iran ilidai kuwa alimchoma kisu afisa wa Walinzi wa Mapinduzi.
Rasaei, anatoka kabila la Wakurdi na Wayaresan ambalo ni kabila la dini ndogo, alikamatwa Novemba 2022 baada ya kushiriki maandamano yaliyopewa jina la “Mwanamke, Maisha, na Uhuru.”
Amnesty International imeelezea kesi yake kama isiyo ya haki kabisa, ikibainisha kuwa ilitumika kama ushahidi wa kulazimishwa kukiri baada ya mateso makali.