Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, anatarajiwa Beijing mwishoni mwa wiki hii wakati kuna hakuna matarajio makubwa ya kuweza kutatua orodha ndefu ya matatizo yanayosababisha ugomvi kati ya Marekani na China.
Blinken na waziri wa mambo ya nje wa China Qin Gang wanatarajiwa kukubaliana namna ya kusuluhisha tofuti zao kupitia mazungumzo.
Blinken atafanya mikutano nchini China kati ya June 18 na 19, na huenda akakutana na rais wa China Xi Jinping.
Atakuwa afisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Marekani kutembelea China tangu rais Joe Biden alipoingia madarakani Januari 2021.
Maafisa wa Marekani hata hivyo, walisema Jumatano kwamba hawana matarajio kwamba ziara hiyo itafikia makubaliano namna Marekani na China zinastahili kushirikiana.
Blinken alizungumza kwa njia ya simu na Qin Gang, Jumanne usiku, ambapo Gang aliiambia Marekani kuacha kuingilia mambo ya ndani ya China.