Umoja wa Ulaya wamwita balozi wake kutoka Niger

Kambi ya jeshi ya Niamey 101 iliyoko Niamey huko Niger. Picha na BERTRAND GUAY / AFP.

Umoja wa Ulaya utamwita balozi wake kutoka Niger baada ya utawala wa  kijeshi wa nchi hiyo kutilia shaka usimamizi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya wa misaada ya kibinadamu iliyokusudiwa kwa waathiriwa wa mafuriko

Umoja wa Ulaya utamwita balozi wake kutoka Niger baada ya utawala wa kijeshi wa nchi hiyo kutilia shaka usimamizi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya wa misaada ya kibinadamu iliyokusudiwa kwa waathiriwa wa mafuriko, Shirika la Huduma za Nje la Ulaya (EEAS) lilisema Jumamosi.

Serikali ya Niger ilitoa taarifa siku ya Ijumaa ikimshutumu balozi wa Umoja wa Ulaya katika nchi hiyo kwa kugawanya fedha za msaada wa Euro milioni 1.3 kusaidia waathiriwa wa mafuriko kati ya mashirika yasiyo ya kiserikali kadhaa ya kimataifa kwa njia isiyo ya uwazi, na bila kushirikiana na mamlaka.

Kutokana na hali hiyo, iliagiza ukaguzi wa menejimenti ya mfuko huo.

Umoja wa Ulaya unaweka wazi kutokubaliana kwake kabisa na madai, pamoja na sababu zilizotolewa na utawala wa mpito, EEAS ilisema katika taarifa yake.

"Kwa hiyo, Umoja wa Ulaya umeamua kumwita balozi wake kutoka Niamey kwa mashauriano mjini Brussels."

Niger imekuwa chini ya utawala wa kijeshi tangu uchukue mamlaka katika mapinduzi ya 2023.