Ukraine iko tayari kwa mazungumzo na Rashia wakati mapigano yakiendelea

Wananchi wakimbia uvamizi wa Rashia dhidi ya Ukraine, wakitembea kwa miguu kuelekea kituo cha mpakani Shehyni kuingia Poland, huku magari yakisubiri kuvuka mpaka nje ya mji wa Mostyska, Ukraine, February 27, 2022

Gari la kijeshi likiwaka moto karibu na magari mengine ya kijeshi yaliyoachwa barabarani wakati wa mapigano kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine wa Kharkiv, Ukraine, Jumapili, Feb. 27, 2022. 

Wanajeshi wa Ukraine wakikagua gari la kijeshi lililoharibika baada ya vita vikali mjini Kharkiv, Ukraine, Jumapili, Feb. 27, 2022. 

Rais Vladimir Putin, wa Rashia, kulia akizungumza na waziri wake wa ulinzi Sergei Shoigu, wapili kushoto, na mkuu wa utawala wa majeshi ya Rashia na naibu wa kwanza wa waziri wa ulinzi, Valery Gerasimov, kushoto, wakati wa mazungumzo yao ya dharura mjini Moscow, Russia, Jumapili, Feb. 27, 2022.

Mwanajeshi wa Ukraine akipita mbele ya mabaki ya gari la kijeshi lililoteketea katika mtaa mmoja wa Kyiv, Ukraine, Feb. 26, 2022.

Watu walokusanyika nje ya Ubalozi mdogo wa Rashia mjini Torornto  Canada katika kupinga uvamizi wa Rashia nchini Ukraine. 

Waandamanaji wakipiga ngomo na kubeba mabango yanayosema  "Russia, stop Putin" wakati wa maandamano mjini Sao Paulo, Brazil, kupinga uvanmizi wa Rashia nchini Ukraine Jumapili, February 26, 2022.

Wakimbizi kutoka Ukraine wakiwasili kwenye kituo cha kuvuka mpaka kwa miguu cha Medyka mjini Przemsyl, mashariki mwa Poland sku ya Jumamosi Feb 26, 2022.

Maandamano ya kupinga uvamizi wa Rashia nchini Ukraine yafanyika mjini Los Angeles, Marekani Jumamosi Feb. 26, 2022.

Rais Volodymyr Zelensky amasema yuko tayari kwa mzungumzo ya amani bila ya masharti yeyote na Rashia kwenye mpaka wake na Belarus katika eneo maalum karibu na Chernobil, baada ya kua na mazungumzo na rais wa Belarus Alexander Lukashenko Jumapili.