Trump kujifikisha kwenye mahakama ya New York Jumatatu

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

Wakati udhibiti wa baadhi ya biashara zake za nyumba ukiwa hatarini, rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema kwamba Jumatatu atafanya hatua isiyo ya kawaida ya kujifikisha kwenye mahakama ya New York.

Trump atafanya hivyo ili kusikilizwa kwa kesi ambayo tayari jaji amesema kwamba alihusika kwenye ufisadi katika baadhi ya shughuli za kibiashara. Kupitia kwenye jukwaa lake la kimitandao la Truth Social, Trump ameandika Jumapili kwamba, “Nitajifikisha mahakamani Jumatatu ili kusafisha jina langu pamoja na hadhi yangu.” Kesi hiyo ni kufuatia uchunguzi uliochukua miaka kadhaa kutoka kwa mkuu wa sheria wa New York Letitia James ambaye anashutumu Trump kwa kudanganya mara kadhaa kuhusu utajiri wake kwenye ripoti za kifedha.