Serikali ya Uholanzi iliamuru China kufunga mara moja vituo vya polisi nchini Uholanzi

Waziri Mkuu wa China Li Keqiang, alipohudhuria mkutano na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte, katika Ukumbi Mkuu wa Watu huko Beijing Juni 27, 2019. (Fred Dufour AP).

Serikali ya Uholanzi siku ya Jumanne iliiamuru China kufunga mara moja "vituo vya polisi" nchini Uholanzi, ambavyo ripoti zinasema vilitumiwa kuwanyanyasa wapinzani.

Vituo vya polisi huko Amsterdam na Rotterdam vilidaiwa kutoa usaidizi wa kidiplomasia lakini vilikuwa havijatoa taarifa kwa serikali ya Uholanzi, vyombo vya habari vya Uholanzi viliripoti mwezi uliopita.

Ripoti hizo zilifuatia uchunguzi wa shirika lisilo la kiserikali la Safeguard Defenders lenye makao yake nchini Uhispania mwezi Septemba, ambalo lilisema China imefungua vituo 54 vya polisi nje ya nchi vikiwemo viwili nchini Uholanzi.

Pia ilisema kulikuwa na vitatu nchini Uingereza na vitatu nchini Canada.

Kwa sababu hakuna ruhusa iliyoombwa kutoka Uholanzi" kwa ajili ya vituo hivyo, "wizara ilimjulisha balozi wa China kwamba ni lazima vituo vifungwe mara moja," Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Wopke Hoekstra alisema kwenye Twitter.