Russia yasema itaendelea na operesheni maalum Ukraine

Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu

Russia imeonyesha ishara Jumanne kuwa inajiandaa na vita virefu nchini Ukraine huku mzozo huo ukiingia mwezi wa nne kukiwa na mapigano makali upande wa mashariki lakini kuna dalili za hali ya kawaida kurejea kwingineko.

“ tutaendelea na operesheni maalumu za kijeshi hadi tutakapofanikisha malengo yote, alisema hayo Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu akitumia jina la Moscow kwa ajili ya vita.”

Miezi mitatu baada ya uvamizi wa Moscow, ufadhili wa Magharibi wa fedha na silaha uliisaidia vimesaidia Ukraine kumzuiya jirani yake kuingia katika maeneo mengi ikiwemo mji mkuu wa Kyiv.

Russia hivi sasa inalenga kulinda na kupanua mafanikio yake katika eneo la mashariki la mkoa wa Donbas karibu na mpaka na makazi ya wa- Russia wanaotaka kujitenga pamoja na ufukwe wa kusini.

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba ameonya kuwa mashambulizi ya Russia huko Donbas ni vita vya ukatili mkubwa Ulaya tangu vita vya pili vya dunia.