Russia inalenga kuharibu kila kitu Donbas, Ukraine - Zelensky

Vifaru vya Russia

Rais wa Ukraie Volodymyr Zelensky amesema kwamba itaendelea kupigana nchini Ukraie kwa mda mrefu hadi ‘kila kitu kitakapoharibiwa Donbas’.

Waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu, amesema kwamba “tutaendelea na oparesheni hiyo maalum ya kijeshi hadi tutakapotimiza malengo yetu.”

Amesema hayo wakati vita hivyo vikiigia mwezi wa nne, huku mapigano makali yakiendelea mashariki mwa Ukraie japo kuna hali ya utulivu katika sehemu zingine za nchi.

Msaada wa silaha na pesa kutoka nchi za magharibi kwa Ukraine, umesaidia nchi hiyo kupambana na wanajeshi wa Russia na kuwazuia kudhibithi sehemu kadhaa za nchi hiyo, ikiwemo jiji kuu la Kyiv.

Russia inalenga kudhibithi kabisa na kupanua udhibithi wake mashariki mwa Donbas, karibu na mpaka unaodhibitiwa na wapiganaji wanaoungwa mkono na Russia, Pamoja na pwani ya kusini.


Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba, ameonya kwamba “mashambulizi ya Russia yanayoendelea Donbas ni mabaya sana, yakiwa makubwa zaidi Ulaya tangu vita vya pili vya dunia.”